Wauza bidhaa za umemenuru shikamaneni kulinda soko

INAWEZEKANA kulinda soko la ndani la bidhaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na za umemenuru, kwa sababu tayari zina kiwango cha ubora kinachoelekeza ni ipi inafaa kwa matumizi na ipi haipaswi kutumika, kwa sababu zipi.

Watumiaji wa umemenuru watakuwa mashahidi wazuri wa kinachoendelea sokoni, ambapo baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakitumia mwanya wa kutofahamika kwa kiwango cha ubora wa bidhaa za nishati hiyo kuwauzia wateja zilizo hafifu na kuwasababishia hasara.

Hivi karibuni Ofisa Viwango wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Henry Massawe, alisema kuwa tofauti na kipindi cha miaka ya nyuma, siku hizi bidhaa za umeme nuru zimekuwa zikiingia kwa wingi nchini kutokana na mahitaji ya watu wengi.

Alisema bidhaa hizo zinazotumika kama mbadala wa nishati ya umeme wa maji ambao Tanzania inautumia zaidi, zimesambaa hadi vijijini ambako ndiko kwenye idadi kubwa ya watu, wanaokadiriwa kufikia asilimia karibu 80 hivyo kuhitaji umakini wa hali ya juu katika matengenezo yake, kuepusha wengi wasiingie k w e n y e m k u m b o wa kupata hasara kwa k u n u n u a zilizo hafifu.

B a a d a ya kuona umuhimu wa kuwa na kiwango kitakachotumika kudhibiti ubora wa bidhaa za umemenuru, ili kulinda soko la ndani la umeme huo, TBS imeandaa kiwango cha kitaifa TZS 1951-9-5:2016 kilichohuishwa kutoka katika kiwango cha kimataifa, yaani IEC 62257-9-5 :2016. Kwa maelezo ya mtaalamu huyo wa viwango, kiwango hicho ni kwa ajili ya bidhaa zote za umemenuru wenye uwezo wa kutoa Wati 15.