loader
Picha

90% ya Watanzania wategemea mkaa, kuni

ZAIDI ya asilimia 90 ya Watanzania hutegemea mkaa na kuni kama chanzo kikuu cha nishati ya kupikia.

Hata hivyo, nishati hiyo inategemewa zaidi na wananchi wenye kipato cha chini katika maeneo ya vijijini suala ambalo linasababisha ukataji wa miti kwa ajili ya mkaa kuwa mkubwa na kusababisha umaskini.

Ofisa Misitu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Alexander Kabado amewataka wananchi mkoani humo kutojihusisha na uchomaji misitu na atakayejihusisha na uharibifu wa mazingira sheria itafuata mkondo.

Akizungumza ofisini kwake, Kabago alisema kumekuwa na tabia sugu kwa baadhi ya watu kujihusisha na uchomaji misitu kwa shughuli za kibinadamu hali ambayo alisema haikubaliki.

"Niwaambie kuwa sheria itafuata mkondo wake kwa atakayehusika na uharibifu wa misitu, kwani elimu imeshatolewa ya kutosha kama watu kusikia wamesikia kinachofanyika ni uzembe tu," amesema.

Hata hivyo alisema, licha ya kuwepo faini ya Sh 50,000 kwa waharibifu wa misitu, bado wanaendelea na uchomaji mkaa katika misitu na kukata miti kwa matumizi mengine.

Kabado alisema, ukataji wa miti hovyo katika misitu kunaweza kuleta majanga likiwemo la ukame na kusababisha uhaba wa mvua hali ambayo inachangia uhaba wa chakula katika baadhi ya maeneo.

Aidha, alisema asilimia 75 hadi 80 ya Watanzania wanategemea kilimo na ufugaji ambao unategemea mvua.

Alisema kunapotokea uhaba wa mvua shughuli za kilimo zinakuwa duni.

Ofisa misitu huyo aliwataka wananchi hususani wakazi wa Dodoma kutumia nishati mbadala kama vile gesi na ikishindikana, watumie meko yanayotumia mkaa kidogo na kuni kunusuru misitu kwa maendeleo endelevu.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi