loader
Picha

Waziri- Marufuku kuuza damu

WIZARA ya Afya imepiga marufuku hospitali zote za serikali nchini kuuza damu na pia imewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa (RMO) na Wilaya (DMO) kutenga siku tatu katika mwaka kuhakikisha wanakusanya damu.

Waganga hao wanatakiwa kuhakikisha damu haiuzwi na waweke mpango mkakati kuhakikisha damu inakusanywa.

Akizungumza jijini Dodoma jana, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani yanayofanyika kitaifa jijini hapo leo, alisema viongozi hao wanatakiwa kusimamia na kuhakikisha hakuna damu inayouzwa kwa wahitaji.

Waziri Ummy alisema katika kuhakikisha damu inapatikana kwa wingi wizara hiyo imeweka lengo la kukusanya chupa za damu salama 375,203 ambazo ni sawa asilimia 60 ya mahitaji ya damu nchini.

Ukusanyaji wa damu ni sawa na chupa saba kwa kila wananchi 1,000 kiwango ambacho ni kidogo ukilinganisha na pendekezo la Shirika la Afya la Dunia (WHO) la kukusanya chupa 10 kwa kila wananchi 1,000.

Ummy alisema katika kipindi cha mwaka 2016 zilikusanywa chupa 196,735 sawa na asilimia 40 ya mahitaji na mwaka 2017 ziliongezeka na kufikia chupa 233,953 sawa na asilimia 45.

"Kwa taarifa za Mpango wa Taifa wa Damu Salama ya mwaka 2017, mikoa iliyoongoza katika makusanyo ya damu ni Katavi ambayo ilikusanya asilimia 94 ya malengo," alisema na kuongeza:

"Mikoa mingine ni Lindi iliyokusanya asilimia 79 ya lengo na Pwani iliyokusanya asilimia 66 ya lengo."

Alitaja mikoa iliyofanya vibaya katika ukusanyaji damu kuwa ni Songwe ambayo ilikusanya asilimia 16 ya lengo, Mbeya asilimia 20 na Tabora asilimia 22 ya malengo.

Alisema mwaka huu serikali imetenga Sh bilioni tatu kwa ajili ya upatikanaji wa damu salama, lengo ni kuongeza upatikanaji damu salama nchini. Ummy alisema mwaka 2017/18, ilitenga Sh bilioni tatu ambazo sawa na ongezeko la asilimia 50 kutoka za mwaka 2016/17 Sh bilioni mbili.

Akizungumzia Meneja wa Mpango wa Damu Salama nchini, Dk Magdalena Lyimo alisema kaulimbiu ya kuwa mwokozi wa maisha, jiunge na kikundi cha wachangia damu wenye kundi adimu la damu inalenga kuweka msukumo kuwa na uwezo wa kupatikana kwa damu hiyo kwa kuunda vikundi.

"Vikundi vitakavyoundwa vinalenga wachangia damu ya makundi adimu kama O hasi, A hasi, B hasi na AB hasi ili kuwa na uhakika wa kuwa na akiba ya kutosha ya damu ya makundi hayo," alisema.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi