loader
Picha

Wasiosoma miaka 7 msingi kubanwa

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Joyce Ndalichako amesisitiza kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Elimu ya mwaka 1978, elimu ya msingi ya lazima ni kwa muda wa miaka saba, na si miaka sita.

Alisisitiza pia kuwa hakuna Waraka wowote uliotolewa na serikali hadi sasa kubadilisha mpango wa miaka 7 kwa ngazi hiyo. Pia, amesema Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 Sura 353 haijabadilishwa na kwamba hakuna mkanganyiko wowote kwa sasa.

Alilazimika kutoa ufafanuzi huo, kutokana na swali la msingi na nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo (Chadema). Katika swali lake la msingi, Suzan alihoji, "Sera ya Elimu ya mwaka 2014 inatambua elimu ya msingi kuwa ya lazima bila malipo. Je, serikali inaweza kuliambia Bunge hili na Taifa kwa ujumla ni lini ulazima huu utatekelezwa kwa vitendo?"

Katika swali lake la nyongeza, Suzan alisema kuna mkanganyiko hivi sasa kwani wakati bado kuna Sheria ya Elimu ya mwaka 1978, kuna Waraka umetolewa hivi karibuni unaoeleza kuwa elimu ya lazima kwa shule za msingi ni miaka 6, badala ya miaka 7.

Suzan alisema yeye ameelezwa na baadhi ya walimu kwamba wanao waraka huo na wameanza kufundisha watoto mitaala inayoishia darasa la 6, badala la darasa la 7.

Aliitaka serikali kuufuta waraka huo, kama inasema Sheria ya Elimu haijabadilika. Akijibu, Profesa Ndalichako alisisitiza kuwa hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika na hakuna Waraka huo, aliodai mbunge Suzan.

"Sheria haijabadilika na hakuna waraka wowote ulioandikwa na kusambazwa kwamba elimu ya msingi ni miaka sita. “Hakuna mkanganyiko wowote, kama mtu anasema kuna mkanganyiko, basi anajichanganya mwenyewe. Vile vile, hakuna waraka wa kuufuta, kwa sababu haupo," alisema Ndalichako.

Awali, akijibu swali la msingi, Naibu Waziri wa Elimu, William Ole Nasha alisema elimu ya msingi ni miaka saba kama inavyoelekezwa na Sheria ya Elimu.

Alisema serikali imeweka kipaumbele cha kuhakikisha kuwa kuna fursa sawa ya kupata elimu. Alisema serikali inaendelea kutekeleza mpango wa elimu ya msingi kuwa ya lazima kwa vitendo tangu 2015/2016.

CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa) Zanzibar kimesema wakati ...

foto
Mwandishi: Nelson Goima, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi