loader
Picha

Maelfu wachaguliwa kujiunga kidato cha tano, vyuo vya ufundi

JUMLA ya wanafunzi 70,904 kati ya 92,712 wenye sifa, wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya Ufundi na eimu kati kwa mwaka 2018 huku wanafunzi 21,808 wakikosa nafasi.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi, jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo alisema kati ya waliochaguliwa, wasichana ni 31,884 na wavulana ni 39,020.

Alisema wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka 2018 ni 58,927 ambapo kati yao wasichana 26,882 na wavulana 32,045.

“ Kati ya waliochaguliwa wanafunzi 30,317 wakiwemo wasichana 11,505 na wavulana 18,812 sawa na asilimia 51.4 watajiunga kusoma masomo ya tahasusi za sayansi na hisabati huku wanafunzi 28,610 wakiwemo wasichana 15,377 na wavulana 13,233 sawa na asilimia 48,6 wamechaguliwa kusoma tahasusi za masomo ya sanaa na biashara.”

Aliongeza: "Wanafunzi 48 kati ya waliochaguliwa wana mahitaji maalumu wakiwemo wasichana 14 na wavulana 34 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano.”

Aidha, Jafo alisema shule shule 354 zikiwemo shule 9 mpya zimepangiwa wanafunzi wa Kidato cha tano, mwaka huu.

Kuhusu Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya ufundi mwaka 2018, Jafo alisema wanafunzi 885 wakiwemo wasichana 173 na wavulana 712 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya ufundi  ambavyo ni chuo cha ufundi Arusha (ATC) Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT), Chuo cha Usimamizi wa Maendeleo ya Maji (WDMI) na Chuo Kikuuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

Jafo alisema wanafunzi 11,977 wakiwamo wasichana 5,002 na wavulana 6,975 waliochaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali katika ngazi ya astashada ya awali, astashahada na stashahada katika vyuo vya Elimu Kati vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) mwaka 2018

Wanafunzi 2,525 wamechanguliwa kujiunga na vyuo vya afya, 4,697 vyuo vya ualimu, 440 (kilimo), 464 (ardhi Tabora na Morogoro), 2,850 (Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo) na 1,000 (Chuo cha Taifa cha Utalii).

Aidha, Jafo alisema kuwa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano wanatakiwa kuripoti shuleni kuanzia Julai 15, 2018 na mwanafunzi atachelewa kuripoti shuleni ndani ya siku 14 nafasi yake atapatiwa mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi hiyo.

“ Fomu za wanafunzi hao kujiunga na kidato cha tano zinapatikana kupitia anuani ya www.tamisemi.go.tz . Sasa hatutaki sababu ya kuwa nilichelewa kupata join instruction (fomu za kujiunga).

Jafo aliongeza: “Kwa kuwa uchaguzi wa wanafunzi ulizingatia ufaulu na nafasi zilizopo katika shule hakutakuwa na fursa ya kufanya mabadiliko yeyote ya shule kutokana na ukosefu wa nafasi kwenye shule husika.”

Kwa upande wa wanafunzi waliopangwa kwenye vyuo vya kati, Jafo alisema kuwa wanatakiwa kuthibitisha kujiunga na kozi pamoja na vyuo walivyochaguliwa kuanzia Juni 16, hadi Agoti 8, 2018 kwa njia ya mtandao.

“Kupitia tovuti ya ya baraza la Taifa la elimu ya ufundi (NACTE) yawww.nacte.go.tz kupitia kiunganishi kinachoitwa  utumishi Tamisemi,” alisema

CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa) Zanzibar kimesema wakati ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi