loader
Picha

Serikali yamwaga ajira 4,985 kwa walimu

SERIKALI inatarajia kuajiri walimu 4,785 wa shule za msingi na 200 wa sekondari. Akihutubia Bunge wakati wa kuahirisha Mkutano wa 11 wa Bunge, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema walimu 4,785 watakaoajiriwa kwa ajili ya shule za msingi watapelekwa kwenye shule zenye mahitaji makubwa na kuwa hatua hiyo ni katika kuimarisha sekta ya elimu nchini.

Alisema tayari serikali imetangaza nafasi za ajira za walimu 200 wa masomo ya sayansi, hisabati na lugha ambao watapangwa kwenye shule za sekondari zenye uhitaji mkubwa. Aidha, Majaliwa alisema Serikali pia imetangaza nafasi za ajira kwa mafundi sanifu maabara 160 ambao pia watapelekwa kwenye shule zenye uhaba wa wataalamu hao. “Serikali inatambua kutokuwapo miundominu ya kutosha katika shule za msingi na sekondari ambayo imechangiwa na ongezeko la uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza na wale wanaojiunga na kidato cha tano kila mwaka,” alisema.

Alisema serikali kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo kupitia mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) imeendelea kuimarisha miundombinu muhimu kwenye shule mbalimbali zenye uhitaji mkubwa, Majaliwa alisema katika mwaka 2018/2019, serikali imepanga kutumia Sh bilioni 155.58 kwa ajili ya ukarabati wa shule kongwe 25, ununuzi wa vifaa vya maabara, ujenzi wa mabwalo 85, vyumba vya madarasa 2,000 na motisha kwa halmashauri kutokana na ufanisi katika utekelezaji wa mradi huo.

Msaada wa kisheria Majaliwa amewataka wabunge kuhamasisha wananchi katika majimbo yao kutumia wasajili wasaidizi ili kupata haki zao za kisheria. Alisema katika kusogeza huduma ya msaada wa kisheria katika ngazi za mikoa, majiji, wilaya na halmashauri zote nchini serikali imeteua wasajili wasaidizi ambao watatoa huduma ya msaada wa kisheria kwa jamii. “Nawaasa wale wote ambao wamepewa dhamana ya kusimamia utaratibu huu wa kutoa huduma kufanya kazi kwa weledi na maadili ili huduma hii iwe endelevu na imsaidie mwananchi wa kawaida aweze kupata haki yake,” alisema.

CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa) Zanzibar kimesema wakati ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi