loader
Picha

Bunge kuzuia Rais kurejesha makao makuu Dar

SPIKA Job Ndugai amesema Bunge litahakikisha linatengeneza Sheria ya Tamko la Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi ambayo haitakuwa rahisi kukanyagwa na kubadilishwa.

Akizungumza jijini hapa, Ndugai alisema baada ya serikali kusoma kwa mara ya kwanza Muswada wa Tamko la Makao Makuu ya mwaka 2018, wao kama Bunge katika vikao vya Septemba watatengeneza sheria madhubuti. “ Haijalishi sheria itakuwa na ukurasa moja, jambo la msingi iwe na kipengele kinachotamka Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi kisheria.

Suala hili limekuwa katika Ilani ya CCM kwa miaka mingi hivyo tunataka kutunga sheria ambayo si rahisi kukanyagwa na kuibadili,” alisema. Alisema kupitishwa kwa sheria hiyo kutaifanya azma ya serikali kuhamia Dodoma ikamilike. Ndugai alihimiza sekta binafsi kusaidia kuijenga Dodoma badala ya kuiachia serikali pekee na kusisitiza ni vyema kuhakikisha linakuwa jiji la kisasa ambalo ni mahususi kwa watu aina zote.

Muda mfupi baada ya kuapishwa mwaka 2015, Rais John Magufuli alitangaza serikali yake kuhamia Dodoma na Aprili 26 mwaka huu akatangaza Dodoma kuwa jiji na kutaka wizara husika kupeleka muswada bungeni ili iwepo kisheria. Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi alipongeza hatua ya serikali ya kuja na muswada huo na kuwa Dodoma inakidhi sifa zote za kuwa Jiji na makao makuu ya nchi hii.

Alisema katika ukusanyaji mapato, Dodoma inaongoza kwa kukusanya Sh bilioni 20 huku mwaka huu ikiwa imekusanya Sh bilioni 210 hivyo kuvuka lengo la zaidi ya asilimia 100. Kunambi alisema pia Dodoma ina wakazi zaidi ya 500,000 idadi ambayo inalifaa kuwa Jiji. Meya wa Jiji la Dodoma, Prof Davis Mwamfupe alisema lengo lao ni kuona Dodoma inakuwa Jiji la huduma kwa kuwa na huduma za jamii za kiwango cha kimataifa ikiwamo elimu na afya.

CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa) Zanzibar kimesema wakati ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi