loader
Picha

Mtoto ajiua kwa bastola

Mtoto mwenye umri wa miaka miwili nchini Marekani, Christopher Williams Jr. amekufa baada ya kujipiga risasi kichwani nyumbani kwao.

Mtoto huyo amejiua kwa kutumia bastola ya baba yake mzazi. Polisi wa eneo la Houston, Texas lilipotokea tukio hilo wamesema, mtoto huyo alikuta bastola hiyo kwenye kochi sebuleni kwao, akaichukua na kuielekeza kichwani kwake na kisha kuifyatua.

Inadaiwa kuwa, wazazi wa mtoto huyo ambaye alikuwa akifahamika zaidi kwa jina la Junior walikuwa nyumbani wakati tukio hilo likitokea.

Mpaka sasa, haijafahamika kama wazazi hao watafunguliwa mashitaka kutokana na tukio hilo lakini imefahamika kuwa, mwaka 2009 baba wa marehemu Christopher Charles Williams, alikutwa na hatia ya kumiliki bastola kinyume na sheria.

Matukio ya aina hiyo yanadaiwa kutokea mara kwa mara nchini humo. Mkuu wa kitengo cha waathiriwa maalum katika idara ya polisi ya Houston David Angelo amewatoa wito kwa wazazi wenye silaha kuhakikisha wanachukua tahadhari.

CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa) Zanzibar kimesema wakati ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi