loader
Picha

Mwalimu atuhumiwa kubaka mwanafunzi gesti

NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William, Ole Nasha ameagiza kukamatwa kwa mwalimu wa Shule ya Sekondari Loliondo, Erick Kalaliche kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wake wa kidato cha tatu.

Mwalimu huyo kwa sasa amehamia mkoa wa Lindi.

Akizungumza jana katika kikao cha dharura kilichofanyika katika makao makuu ya Halmashauri ya Ngorongoro, Ole Nasha amesema, jambo hilo linasikitisha na kuidhalilisha sekta ya elimu na lazima hatua za kisheria na kinidhamu zichukuliwe mara moja.

Amesema Wizara ya Elimu haiwezi kuvumilia walimu wanaopachika mimba wanafunzi wanaowafundisha wala wazazi wanaofumbia macho vitendo vichafu ambavyo vinarudisha nyuma sekta ya elimu.

Ofisa Elimu wa wilaya ya Ngorongoro, Emanuel Sukuma amekiri kupokea taarifa ya mwalimu huyo kutenda kosa la kumbaka mwanafunzi mwezi wa tatu ambapo habari zake zilijulikana mwezi wa sita na mpaka sasa hakuna hatua zozote za kinidhamu zilizochukuliwa.

Alisema mwalimu Erick alimchukua mwanafunzi huyo ambaye alikuwa anasoma kidato cha tatu katika shule hiyo ya Sekondari Loliondo na kumpeleka nyumba ya kulala wageni na kumbaka.

Ole Nasha amefanya ziara ya kushtukiza shule ya sekondari Loliondo na kuhoji kuhusiana taarifa za mwalimu huyo. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Neema Mchao amekosa majibu sahihi mbele ya Naibu Waziri lakini baadaye kukiri kwamba mwalimu alihama shule.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Loliondo, Mchao amekiri kufuatilia jambo hilo lakini alipohojiwa kwa nini hakuchukua hatua za kinidhamu alisema yeye aliachia mamlaka husika kwa sababu hata yeye jambo hilo lilimsikitisha.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye ni mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Rashidi Taka amesema utaratibu unafanyika kurudishwa kwa mwalimu huyo kutoka mkoa alikohamishiwa.

CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa) Zanzibar kimesema wakati ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi