loader
Picha

Bendera zamkera Waziri Mpango

WAZIRI wa Fedha, Philip Mpango ametaka Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) kuhakikisha wanabadili bendera zilizochakaa zinazopeperushwa katika magari ya viongozi.

Mpango amesema GPSA wasipotekeleza atachukua hatua.

Amesema, alishawapigia simu kuhusu ubora wa bendera hizo lakini hali bado ipo hivyohivyo.

Ametoa agizo hilo alipotembelea banda la wizara yake lililo na taasisi zilizo chini yake katika Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Sabasaba.

“Sitaki kuona hali hii tena vinginevyo nitachukua hatua kwani si nilishawapigia simu kuwaeleza ubora wa bendera zinazopepea katika magari ya mawaziri, nyingi zimechanika ikiwemo yangu na kubaki nyuzi tu,” alisema.

Waziri amesema bendera ni alama ya taifa inayohitaji heshima na watanzania wanahitaji kuona alama hizo zikiwa na ubora ni vema kuangalia zote zilizopo barabarani kuhakikisha hakuna inayopepea ikiwa imechanika.

“Unakuta waziri akinunua bendera na kutembea kutoka Kibaha mpaka Chanika inakuwa imeshachanika"amesema.

Awali alipotembelea banda la bodi ya wataalamu wa masuala ya manunuzi na ugavi (PSPTB) alisema sheria ya kuwabana wataalamu wa masuala ya ununuzi na usambazaji vifaa bado siyo kali kama anavyotaka ni vema waharibifu kutangazwa kwa umma.

Amesema wananchi wanavuja jasho kwa ajili ya kulipa kodi wakiwemo wengine wanatia huruma katika kulipa kodi huku wachache wakizila pesa hizo ndani ya serikali hivyo ni vema bodi hiyo kusimamia kwa nguvu wataalamu wao serikalini, kwani pesa nyingi za serikali zinapotea katika taaluma hiyo.

Mpango aliwataka kujiongeza kiteknolojia kwani wajanja wanawazidi maarifa kila wanapobuni njia za mtandao ili kuwadhibiti huku akitaka kupata orodha ya waharibifu katika makampuni wanayosimamia.

CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa) Zanzibar kimesema wakati ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi