loader
Picha

Serikali kufumua mfumo shehena bandarini

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa wakuu wa taasisi za serikali, wanaohusika na udhibiti wa mizigo katika maeneo hayo na wadau wa sekta binafsi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Charles Kichere amesema lengo la kuwashirikisha wakuu hao ni kujenga uelewa wa pamoja wa utekelezaji wa mfumo huo.

"Uwepo wenu katika mkutano huu ni muhimu sana kwa sababu mtaweza kupitia mahitaji yote ya mfumo yaliyoandaliwa na wataalamu wetu ikiwa ni pamoja na maeneo ya kisheria, kiufundi na kibiashara ili muweze kuuboresha zaidi," amesema Kichere.

Kichere amesema, uwepo wa wakuu hao na wadau wa sekta binafsi katika mkutano huo ni kiashiria cha kuunga mkono azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga mazingira bora ya kufanya biashara ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Amesema, Serikali imelenga kuwawezesha wadau wote wanaohusika na biashara za kimataifa na usafirishaji wa mizigo kutumia Mfumo wa Pamoja wa Kielektroniki wa Uondoshaji Shehena, kwa lengo la kuwezesha uwasilishaji wa nyaraka mahali pamoja ili wadau wote waweze kushughulikia nyaraka hizo kwa wakati.

Mratibu wa Mfumo huo kutoka TRA, Felix Tinka ametaja faida za mfumo huo kuwa ni kurahisisha na kuwezesha biashara, kuongeza ufanisi wa matumizi bora ya rasilimali na kuongeza uhiari wa ulipaji ushuru na tozo mbalimbali kwa waingizaji na waondoshaji wa mizigo.

"Mfumo huu una faida nyingi, mbali na hizo nilizozitaja awali, pia kuna kuimarisha usalama, kuimarisha uadilifu na uwazi katika utendaji kazi, kupunguza biashara haramu, kupunguza gharama, kupunguza muda wa uondoshaji mizigo katika vituo vya forodha pamoja na kurahisisha ufuatiliaji wa mizigo kwa wakati," amesema Tinka.

Utekelezaji wa Mfumo huo umegawanyika katika maeneo makuu matano ambayo ni eneo la usimamizi wa mapato, uwezeshaji wa usafiri na uchukuzi, utekelezaji wa sera na biashara, na usimamizi wa afya na usalama wa umma, usalama wa uchumi pamoja na ugawaji.

MKUU wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel amewakaribisha wananchi wa ...

foto
Mwandishi: Veronica Kazimoto

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi