BUNGE Maalumu la Katiba, limepitisha marekebisho ya Kanuni zake, ili kutoa fursa kwa wajumbe wa Bunge hilo kupiga kura ya kukubali au kukataa Katiba inayopendekezwa, mahali popote walipo hata nje ya nchi katika muda mfupi kwa kutumia nukushi (faksi) au intaneti.
zaidi ya miaka 7 iliyopita
WATU wenye hasira wamempiga hadi kumuua mwanamume, aliyemuua mke wake kwa kumpiga rungu tumboni.
LICHA ya kutakiwa kufuata taratibu kabla ya kutimiza azma yao ya kuandamana nchi nzima, viongozi wa Chadema wa mikoa mbalimbali wamesisitiza kuendelea kuunga mkono dhamira ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe ya kuandamana na kugoma bila kikomo ili kulipinga Bunge Maalumu la Katiba, linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma.
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva amesema uboreshaji wa Daftari la Wapigakura umechelewa kuanza kutokana na kuchelewa kuagiza vifaa vya kufanya kazi hiyo kwa wakati, hivyo kazi hiyo sasa itafanyika mapema mwakani.
AMRI ya kutotoka nje iliyowekwa nchini Sierra Leone ya siku tatu kwa ajili ya kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa ebola, imeonekana kufanikiwa.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zantel imesema itaendelea kuboresha huduma zake katika mikoa yote nchini ili wananchi wanufaike zaidi.
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana imetupilia mbali pingamizi la awali lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) dhidi ya kesi ya kikatiba inayohoji uhalali wa Bunge Maalumu la Katiba iliyofunguliwa na Mwandishi wa Habari, Said Kubenea.
TAASISI ya Wahandisi Tanzania (IET) imeshauri Serikali kuanzisha kampeni za kuhamasisha masomo ya sayansi na teknolojia katika shule za msingi na sekondari kuwezesha taifa kuwa na wataalamu wa kutosha kutoka katika eneo hilo.
MAHABUSU wanaokabiliwa na kesi za mauaji kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana waligoma kushuka kwenye basi la Magereza kwa madai kwamba kesi zao zinachukua muda mrefu na upelelezi hauishi. Kutokana na mgomo huo, walirudishwa kwenye Gereza la Kisongo mkoani hapa.