WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amewataka watu waliopata elimu kuitumia kwa manufaa ya umma ili kuleta mabadiliko ya haraka katika jamii.
zaidi ya miaka 8 iliyopita
WA K A Z I wawili wa kijiji cha Kakese, John M w a k a l e - bene (24) na Kamili Lugoye (30) wametiwa hatiani na kuhukumiwa na makakama ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi kwenda jela miaka 60 baada ya kupatikana na hatia ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
JUMLA ya Sh milioni 107, zimeokolewa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Tabora, ambazo zilikuwa zitumike katika manunuzi hewa kwenye ofisi mbali mbali za Serikali.
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linafanya uchunguzi kuhusu tukio la mume na mke kumshambulia mtalaka wake Faustina Komba (35) mkazi wa jiji la mbeya kwa kumpiga ngumi, makofi na kumng’ata mdomo wake wa chini na kuuondoa wote.
MBUNGE wa jimbo la Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma, Kabwe Zitto amesema kuwa ataendelea kupigania haki yake ya kidemokrasia na uwajibikaji ndani ya chama chake hadi dakika za mwisho.
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,kuanzia mwaka huu imeanza kutumia mfumo wa kielektroniki kwa wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza.
SIKU ya maziko rasmi ya kiongozi wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela katika kijiji alichokulia cha Qunu, jimboni Eastern Cape, Desemba 15, hakuna mtu aliyeshuhudia mila zikifanyika nje ya wanafamilia.
WABUNGE wamepongeza hatua ya mawaziri wanne kukubali kujiuzulu na kuundwa kwa Tume ya Uchunguzi wa Kimahakama, kwa sababu itawasaidia kuwapoza wananchi ama kuondoa machungu yaliyotokana na Operesheni Tokomeza Ujangili.
WATUMISHI 866 wa serikali wamechukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria kwa ubadhirifu wa fedha katika halmashauri mbalimbali nchini.
USIKU wa Ijumaa Desemba 20, Watanzania walishuhudia kutenguliwa kwa uteuzi wa mawaziri wanne baada ya Rais Jakaya Kikwete kukubaliana na kilio cha wabunge cha kumtaka awawajibishe mawaziri hao kutokana na makovu mabaya yaliyotokana na Operesheni Tokomeza Ujangili.