ALIYEWAHI kugombea ubunge wa Mlalo Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwaka 2005, Charles Kagonji amekihama chama hicho na kurejea katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).
zaidi ya miaka 7 iliyopita
RASIMU ya tatu ya Katiba maarufu kama Rasimu ya Sitta ambayo leo inaanza kupigiwa kura imejikita katika kutetea mahitaji na maslahi mahususi ya makundi makubwa ya jamii ili ikubalike kirahisi.
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo amewataka askari wa Usalama Barabara (trafiki), kuacha kuwa na huruma nyingi pale wanapokamata magari yenye matatizo.
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji umeme wa msongo mkubwa, kilovoti 400 itakamilika pasipo shaka ifikapo June 2016.
WATANZANIA wameombwa kuongeza uelewa kuhusu magonjwa ya moyo, wanapoadhimisha Siku ya Moyo Duniani leo.
SIKU chache baada ya Bunge Maalumu la Katiba (BMK) kupokea rasimu ya Katiba mpya iliyopendekezwa, mmoja wa wajumbe wa bunge hilo anayetoka kundi la 201, John Ndumbaro ameibukia mjini hapa na kutaka vipengele kadhaa vifanyiwe marekebisho.
MAKAMU Mwenyekiti Taifa kupitia Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Patrick ole Sosopi ametoa wito kwa wanachama wa chama hicho, kushiriki kuchagua au kuchaguliwa katika chaguzi, zitakazofanyika nchini, ukiwemo wa Serikali za Mitaa.
IMEELEZWA kuwa ufanisi wa watumishi katika ngazi mbalimbali za kiutendaji unaweza ukaongezeka pindi wafanyakazi wanapokutana pamoja na kubadilishana mawazo na viongozi wao katika hali ya kirafiki.
OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imewataka watunga sera, taasisi, mashirika ya umma na wadau mbalimbali wa maendeleo kuitumia kanzidata (data base) rasmi ya takwimu za chakula na kilimo iliyoanzishwa kwa lengo kutoa takwimu hizo kutoka katika maeneo mbalimbali.
SERIKALI imewataka watekelezaji wa miradi mbalimbali katika sekta ya maji kuzipa kipaumbele kazi za usimamizi ili ikamilike ndani ya muda uliopangwa kwa mujibu wa mikataba.