SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limezuia shehena 125 zinazotoka nje ya nchi zisiingizwe sokoni, kwa sababu ya kutokidhi viwango vya ubora vya kitaifa na kimataifa.
zaidi ya miaka 7 iliyopita
CHAMA cha Wanawake wa Afrika na Uelewa wa Saratani (AWCAA) kimemkabidhi mke wa Rais, Mama Salma Kikwete mashine moja ya Mammogram, ambayo inatumika kupima ugonjwa wa saratani ya matiti, yenye thamani ya zaidi dola za Marekani 200,000 (Sh milioni 320).
JESHI la Polisi nchini lipo kwenye mchakato wa kuboresha mifumo mbalimbali ya utekelezaji kazi na kutunga sheria mpya ya jeshi hilo ili kukidhi matakwa na hali halisi ya sasa.
MWENYEKITI wa Taifa wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Sadifa Juma ameomba suala la umri wa kugombea Uspika na Urais, liangaliwe ili kuwapa nafasi vijana kuweza kugombea nafasi hizo kwa kupunguza umri wa sasa wa miaka 40 na kuwa 30.
WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) una mpango wa kutumia teknolojia mpya ya kujenga nyumba ya ghorofa kwa siku moja lengo likiwa ni kuisaidia Serikali katika kupunguza uhitaji wa nyumba pamoja na kupunguza gharama za ujenzi.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema hali ya amani na utulivu katika eneo la Afrika Mashariki ni ya kuridhisha.
WAJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba, waliopiga kura ya ‘Hapana’ kwa Rasimu yote ya Katiba Inayopendekezwa, wameundiwa Kamati ya Mashauriano itakayosikiliza malalamiko yao.
MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia ameeleza wasiwasi wa nchi kuhujumiwa iwapo biashara ya gesi itaachwa mikononi mwa wageni pekee.
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linachunguza tukio la askari wake (jina tunalo), iwapo alimtorosha na kumweka kinyumba mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Okaoni, wilayani Moshi Vijijini.
WANAHARAKATI wa masuala ya jinsia na mtandao wa wanawake na Katiba wamepongeza Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa kwa kuingiza madai yao kwa asilimia 90 na kusema kuingia huko kumetokana na wao kuvua itikadi za dini na vyama vyao na kuvaa joho la jinsia na uzalendo.