UJENZI wa miundombinu ya kusafirisha umeme kutoka nchini Kenya kupitia Tanzania mpaka Zambia unaotarajiwa kupunguza bei za umeme kwa nchi husika umeanza, huku mawaziri wa sekta ya nishati kwa nchi husika wakikubaliana kukamilisha mwishoni mwa mwaka 2016.
zaidi ya miaka 7 iliyopita
SERIKALI ya Marekani imepanga kutoa zaidi ya Dola za Marekani milioni 40 kwa Tanzania katika miaka mitano ijayo, kusaidia shughuli mbalimbali za uhifadhi na usimamizi wa wanyamapori nchini.
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amewataka vibarua kwenye Kampuni ya ukandarasi ya India ijulikanayo kwa jina la KEC International Limited inayojenga mradi wa msongo mkubwa wa umeme wa Kilovoti 400 kuacha kuchanganya siasa na uanaharakati kwenye kazi.
MFANYABIASHARA wa mjini Tarime mkoani Mara, Wilson Weso maarufu Kishimba (34) amekufa kwa kile alichodaiwa amekunywa sumu nyumbani kwa baba mkwe wake.
VYUO na taasisi za Canada vinashirikiana na Taasisi za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa ajili ya kuandaa zana za kufuatilia namna ambavyo programu za mafunzo ya ujuzi zinavyowawezesha kuongezeka kwa ajira za vijana katika sekta za mafuta, gesi, uchimbaji wa madini na utalii.
MKUU wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya ametaka vyombo vya habari kujiepusha na kutangaza habari zinazoumiza hisia za wananchi. Aidha alisema uadilifu katika vyombo vya habari kutaepusha migogoro.
RAIA wa Ufaransa, Folkertsma Laurent (41) amepandishwa kizimbani kusomewa maelezo ya awali ya mashitaka yake na kukana kumpiga mfanyakazi wake wa ndani.
MWANAFUNZI wa darasa la tatu shule ya msingi Mnomo Kata ya Msangamkuu, Wilaya ya Mtwara Vijijini, Ahmadi Mtuna (10), amekufa baada ya kujinyonga kwa kamba ya manila katika dari la nyumba aliyokuwa akiishi.
MWENDESHA pikipiki ya magurudumu matatu (bajaj) aliyetambuliwa kwa jina la Temeni Esrom anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35 na 40 amekufa papo hapo baada ya kugongana na gari.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amekosoa tabia ya watendaji wa serikali, kushindwa kuwajibika katika nafasi zao na kusukuma matatizo yote kwa Waziri Mkuu na Rais.