KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime ameeleza siri ya timu ya Zesco United kufanya vizuri kwamba wanacheza kama timu na kikosi hicho kina wachezaji wote wazuri.
zaidi ya miaka 8 iliyopita
BINGWA mtetezi wa mashindano ya Airtel Rising Stars, Mwanza imeanza vibaya mashindano hayo baada ya kuchezea kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Ilala kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Karume Dar es Salaam.
CHELSEA ilitoka kuwa nyuma na kushinda mabao 2-1 dhidi ya Ferencvaros juzi, lakini ilipata pigo baada ya kuumia kwa mshambuliaji Didier Drogba.
ARSENE Wenger amemthitibisha Mikel Arteta kuwa nahodha mpya wa Arsenal baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Manchester City katika Ngao ya Jamii juzi.
TP Mazembe na Vita Club zimesonga mbele katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi katika Kundi A juzi Jumapili. Mabingwa wa mwaka 2009 na 2010, Mazembe iliishinda Al Hilal Omdurman mabao 3-1 na kuhakikisha wanaendelea kuwania taji la tatu katika miaka sita.
HATIMAYE imethibitika kuwa kocha wa zamani wa Simba, Patrick Phiri anatua leo kuja kuanza kazi rasmi baada ya uongozi wa Simba kukubaliana naye.
AZAM FC jana ilijiweka pazuri katika kucheza robo fainali ya Kombe la Kagame baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na timu ya Atlabara ya Sudan Kusini.
TIMU ya wavulana ya Morogoro jana ilifanya mauaji ya maangamizi baada ya kuifunga Mbeya mabao 6-1 katika fainali za taifa za mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
KAMATI ya Mashindano ya Kombe la Majimbo imeyaondoa majimbo matano baada ya kushindwa kukamilisha taratibu za mashindano hayo.
MFUNGAJI anayeshikilia rekodi nchini Ujerumani, Miroslav Klose ametangaza kustaafu soka ya kimataifa. Mshambuliaji huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 36, amefunga mabao 71 katika mechi 137 katika zaidi ya miaka 13 aliyoichezea timu ya Taifa.