KLABU ya Simba imenasa mastraika wengine wawili kutoka Botswana na Gambia watakaochuana na Mkenya Paul Kiongera kujaza nafasi iliyobaki ya mchezaji mmoja wa kigeni msimu ujao.
zaidi ya miaka 6 iliyopita
TIMU ya Jimbo la Makunduchi imeanza vizuri Michuano ya Majimbo kwa kuwatambia mabingwa watetezi, Jimbo la Fuoni baada ya kuwafunga mabao 3-1.
MASHINDANO ya mpira wa magongo ya kimataifa yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo jijini Tanga.
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Mtibwa Sugar, Juma Luizio atakiongoza kikosi cha Zesco United kitakachotua leo mchana kutoka Zambia kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Simba katika Tamasha la Simba kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
CHUO cha Maendeleo ya Michezo Mallya mkoani Mwanza, kimezihimiza halmashauri, taasisi na watu binafsi kuona umuhimu wa kuendeleza michezo kwa kupeleka watu kusoma katika chuo hicho na kuajiri wale wenye ujuzi kwa maendeleo ya michezo.
WAREMBO 12 wanatarajia kupanda jukwaani leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Nashera mjini hapa, kuwania taji ya urembo la Miss Kanda ya Mashariki.
KESI ya mwanariadha maarufu wa Afrika Kusini anayekabiliwa na kosa la mauaji ya mpenzi wake, Oscar Pistorius, itaanza kusikilizwa bila ya kuoneshwa moja kwa moja kwenye luninga (live).
MICHUANO ya soka ya Majimbo yanazidi kupamba moto kisiwani Unguja baada ya juzi timu za majimbo ya Bububu, Mji Mkongwe na Chwaka kushinda.
TIMU ya Magazeti FC imeanza vizuri Kombe la Meya jijini Mwanza baada ya kuichapa timu ya Kata ya Buhongwa mabao 4-1 katika Kituo cha Buhongwa.
MABINGWA wa soka wa Tanzania Bara, Azam FC na wale wa Zanzibar, KMKM, wameanza kwa sare katika michuano ya mwaka huu ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).