TIMU ya soka ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys inatarajiwa kushuka dimbani leo kwenye Uwanja wa Dobsonville, Soweto nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Amajimbos kufuzu michuano ya Afrika kwa vijana.
zaidi ya miaka 7 iliyopita
KLABU ya Simba imewatambulisha wachezaji watatu iliyowasajili kwa ajili ya kuitumkia msimu ujao.
SERIKALI imesema ujio wa makocha wa FC Barcelona nchini, una manufaa katika maendeleo ya michezo na kwamba inaunga mkono jitihada za wadau wenye nia ya kuendeleza michezo.
TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars leo ina kibarua kizito cha kukabiliana na Msumbiji ‘Black Mambas’ katika mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Zimpeto kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani.
MWANARIADHA wa Tanzania, Bazil Boay Baynit ameingia fainali ya mbio za mita 1,500 kwa wanaume katika Michezo ya 20 ya Jumuiya ya Madola inayofikia tamati leo Glasgow jijini Scotland.
MKUTANO Mkuu wa wanachama wa Klabu ya Simba unatarajiwa kunguruma leo kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam ukiwa wa kwanza chini ya uongozi mpya.
MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando leo anatarajia kuzindua albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
WATANZANIA wanaoishi nchini Msumbiji wameonesha matumaini makubwa ya timu ya Taifa (Taifa Stars) kuibuka na ushindi na kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani.
TANZANIA itabidi isubiri kwa miaka mingine mitatu kama inataka kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya jana kutupwa nje ya michuano ya awali.
KATIBU Mkuu wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania (FAT) sasa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura, amefukuzwa uanachama wa klabu ya Simba, kwa tuhuma za kuipeleka mahakamani.