HABARI za leo wapenzi wasomaji wa gazeti la HabariLeo Jumapili. Ni matumaini yangu mmeamka salama na kumtukuza Mungu kwa kuwapa uzima wake leo.
mwaka 1 uliopita
KWA kutambua kuwa ajali za barabarani ni janga kubwa la dunia, Umoja wa Mataifa hivi karibuni ulizindua mfuko wake wa kufanikisha harakati za usalama barabarani ambao lengo lake ni kupambana na janga hilo katika nchi mbalimbali.
BALEHE ni kipindi muhimu katika ukuaji wa mtu kuelekea utu uzima. Hiki ni kipindi cha mabadiliko makubwa ya ki maumbile na kiakili ambayo yanaletwa na mabadiliko katika homoni za jinsia na uzazi.
INANENWA kwamba nchi ya Nigeria yenye watu wengi zaidi Barani Afrika pia inazo sifa mbili kuu; imani kali za ushirikina na idadi kubwa ya makanisa. Nimetumia neno ushirikina kumaanisha uchawi kwa sababu ndivyo wengi hulichukulia neno hilo ingawa kiukweli hiyo ni sehemu ndogo tu ya maana ya ushirikina.
JINSIA tata (ambiguous genitalia) ni neno linalotumika kuelezea viungo vya siri vya mtoto aliyezaliwa ambavyo ni vigumu kujua kama ni vya jinsia ya kike au ya kiume; hali ambayo inaweza kuwa ni kwa sababu viungo hivyo havijakomaa vizuri au mtoto ana viungo vya jinsia zote mbili.
U hali gani mpenzi msomaji wa safu hii, natumaini kwa uwezo wa Mungu uko salama na unaendelea kuwajibika ipasavyo. Leo nimeona tukumbushane habari ya mavazi kama sababu ya MC kupendwa, kuvutia , kupendeza na hivyo kupata kazi nyingi zaidi kutokana na umaridadi wako.
NI jambo la kawaida wengi wetu kuingia kwenye uhusiano, huku tukiwa na matumaini kwamba wenza tulio nao watakidhi vigezo vyetu na hivyo kutufaa katika maisha yetu ya uhusiano.
WAZAZI makini na wenye uchungu na maisha ya baadaye ya watoto wao watakubaliana na safu hii kwamba wanahitaji nguvu ya ziada katika makuzi na malezi ya watoto wao wa kizazi hiki cha dijitali ambacho ndiyo kwanza kimeanza kupamba moto kutupilia mbali mfumo wa analogia uliotulea sisi wazazi wao.
‘NI kama Ulaya.’ Ni kauli inayotolewa na watu wengi (niliokutana nao) waliofika katika Hospitali ya Taaluma na Tiba Mloganzila (MAMC) iliyopo mpakani mwa Kisarawe mkoani Pwani na Ubungo, Dar es Salaam.
JUMAMOSI iliyopita uongozi wa Simba, ulitangaza kuachana na aliyekuwa kocha wake mkuu raia wa Cameroon, Joseph Omog, kufuatia matokeo mabaya ya timu hiyo katika mchezo wa kufuzu hatua ya 32 ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Green Worriors ya daraja la pili.