ZABUNI ya vitalu vya utafiti wa mafuta na gesi asilia vilivyo bahari kuu na Ziwa Tanganyika Kaskazini, inatarajiwa kufungwa Mei 15 mwaka huu. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alisema hayo wakati alipofanya mazungumzo na Waziri mstaafu wa Nishati na Viwanda wa Ufaransa, Erick Besson.