MITAJI ya ubia imetajwa kama mpango unaoweza kuongeza nguvu katika miradi ya wafanyabiashara nchini na kuchangia uchumi na ustawi wa jamii. Akifungua mkutano wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) mwishoni mwa wiki, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu alisema kukubalika kwa mpango wa mitaji ya ubia, ni ishara ya utayari wa Serikali katika kuweka mazingira ya kufanya sekta binafsi kuwa injini ya uchumi hapa nchini.