MJI wa Bagamoyo umetajwa kuwa moja ya maeneo yenye fursa nyingi za uwekezaji na zinavutia kuwekeza katika sekta mbalimbali, ambazo zikitumika ipasavyo zitasaidia mji huo uliopo mkoani Pwani kupiga hatua za haraka kiuchumi. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu alisema hayo jana Bagamoyo, wakati wa ziara ya Meya wa Mji wa Vallejo uliopo Jimbo la California Marekani na wafanyabiashara wa mji huo.