BANK of Africa Tanzania imepata faida ya Sh bilioni 5, mwaka jana kabla ya kodi, ikilinganishwa na faida ya Sh bilioni 3.3 iliyopatikana mwaka juzi. Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Ammish Owusu-Amoah alisema mafanikio hayo, yanatokana na ongezeko la jumla la kipato cha riba, gharama mbalimbali zinazotozwa pamoja na bidhaa za hazina.