PAMOJA na ongezeko la ushindani katika sekta ya kibenki, Benki ya CRDB imeweza kupata faida ya Sh bilioni 84.37 baada ya makato ya kodi katika kipindi cha mwaka ulioishia 2013 ikilinganishwa na Sh bilioni 80.54 zilizopatikana mwaka uliotangulia.
zaidi ya miaka 8 iliyopita
MATUMIZI ya huduma za kifedha nchini yameongezeka na kufikia asilimia 57 ya Watanzania. Idadi hiyo ni kubwa ikilinganishwa na mwaka 2009, ambapo nusu ya Watanzania hawakufikiwa na huduma hiyo. Ongezeko hilo limetajwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
KAMPUNI ya Ndege ya Tanzania (ATCL) imeweka rekodi ya ongezeko la abiria kwa asilimia 57 wiki chake baada ya kupokea ndege ya kukodi yenye uwezo wa kubeba abiria 50 aina ya CRJ-200 pamoja na kuiongezea uwezo wa kuruka kwa wakati kwa asilimia 98.
OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetangaza kuwepo kwa mfumuko wa bei kwa mwezi Machi, kutoka asilimia 6.0 mwezi Februari hadi kufikia asilimia 6.1 Machi mwaka huu. NBS ilieleza kuwa mfumuko huo unamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Machi imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa Februari mwaka huu.
BENKI ya Exim imepata faida ya Sh bilioni 20 kabla ya kodi hadi kuishia Desemba mwaka jana, ikionesha ongezeko la asilimia 21 kutoka Sh bilioni 16.5 iliyopatikana mwaka juzi.
KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ametaka watanzania, hususani wafanyabiashara kujiandaa na kuelewa fursa zinazopatikana katika sekta ya gesi, wafaidike kwa kuwekeza katika maeneo yote, ambako rasIlimali hiyo inachimbwa.
SERIKALI kupitia Mpango wa Kurasimisha Rasilimali wa Biashara (MKURABITA) itatumia zaidi ya Sh milioni 60 kuwapatia wakulima wadogo wa miwa hati za kimila katika vijiji 10 vilivyopo Wilaya za Kilombero na Kilosa mkoani Morogoro.
KAMPUNI ya Tumbaku Tanzania (TLTC) yenye makao yake makuu mjini Morogoro, jana ilitangazwa kuwa Kampuni bora ya mwaka 2014 kwenye tuzo za heshima za Uluguru (Uluguru Awards), zilizofanyika mjini hapa.
JUMUIYA ya Vikundi vya wenye Viwanda na Biashara Ndogo Tanzania (Vibindo), wameitaka Serikali kuondoa ada za leseni au kuzipunguza kufikia viwango ambavyo vitaruhusu biashara hizo kukua.
WAENDESHA vyombo vya moto nchini wamerahisishiwa njia ya kununua na kulipia mafuta kwa njia ya M-Pesa, kufuatia ushirikiano kati ya kampuni ya simu za mkononi Vodacom M-Pesa na kampuni ya uuzaji na usambazaji wa mafuta ya Total Tanzania.