KAMPUNI ya Ndege ya Tanzania(ATCL) imesaini mkataba wa ushirikiano na kampuni ya Interair ya Afrika Kusini, itakayowezesha kampuni hiyo kuwa na safari tatu kwa wiki kati ya Dar es Salaam na Johannesburg, Afrika ya Kusini ikiwa ni kama ratiba ya mwanzo.
zaidi ya miaka 8 iliyopita
WAFANYABIASHARA katika soko la Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam ambao wanadai kupoteza mitaji yao na kuwaacha na madeni katika taasisi za fedha kutokana na moto ulioteketeza soko hilo wamesikitishwa na kitendo cha serikali kutowajali.
SEKTA binafsi nchini imekaribisha wawekezaji kutoka Jamhuri ya Watu wa China kuwekeza nchini kwa faida ya pande zote mbili.
WAWEKEZAJI kutoka China wameshawishiwa kuwekeza katika maeneo ya Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA) ambayo yameshatengwa kwa ajili hiyo katika mikoa mbalimbali.
KAMPUNI ya Tigo imetangaza kuingia katika ushirikiano na kampuni ya Teknolojia ya Huawei ili kuwawezesha wateja wa kampuni hiyo ya simu nchini kuweza kupata simu za kisasa kwa bei nafuu.
SOKO la zao la Ufuta limeanza kuyumba mkoani Lindi ambapo wanunuzi wananunua kilo moja kati ya Sh 2,000 na 2,300 badala ya Sh 2,500 iliyopangwa na serikali.
SERIKALI imesema ipo haja ya kuwekeza katika sekta ambazo wananchi wengi ndipo walipo ili waweze kunufaika na kukua kwa uchumi pamoja na kupunguza umasikini.
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ametembelea Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara na kueleza kutoridhishwa na ubora na mvuto wa eneo la maonesho.
WAKATI Chuo Kikuu cha Ardhi kikiibuka na ushindi wa jumla katika tuzo za maonesho ya Sabasaba, Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) nalo limeibuka kidedea katika kundi la huduma bora za pensheni na bima.
WATANZANIA wametakiwa kuthamini na kutumia bidhaa hususani samani, zinazozalishwa na Jeshi la Magereza nchini.