BENKI M Tanzania imeweka rekodi baada ya kupata faida kabla ya kodi hadi kufikia asilimia tisa katika robo ya mwaka iliyoishia Juni 2014.
zaidi ya miaka 7 iliyopita
WAKULIMA wa pamba Kanda ya Ziwa waliopata hasara baada ya kutumia mbegu mpya ya pamba aina ya Quton, wameitaka Bodi ya Pamba (TCB) hapa nchini kuhakikisha inawalipa fidia kutokana na hasara hiyo.
WAZIRI wa Fedha, Saada Mkuya, ameagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), uimarishe usimamizi na udhibiti wa manunuzi makubwa yanayofanyika Serikalini, ili kuzuia ubadhirifu unaoliingizia taifa hasara.
ZAIDI ya tani za karafuu 7,373 zenye thamani ya Sh bilioni 76.0 zimenunuliwa kutoka kwa wakulima katika msimu wa mavuno uliopita wa mwaka 2013-2014 na kuvuka malengo yaliyowekwa awali ya kununua tani 4,200.
DHAMANA ya Uwekezaji Tanzania (UTT) imeanza kutumia huduma ya MPesa katika kuwawezesha watanzania kununua vipande vya mifuko ya pamoja iliyopo chini ya UTT.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kutekeleza uamuzi wake wa kuwapatia wakulima bei ya karafuu ya asilimia 80 ya bei ya zao hilo katika soko la nje.
KAMPUNI ya kimataifa ya Methanex ya Canada, inayotengeneza na kusafirisha malighafi ya methano imesema Tanzania ni moja ya maeneo muhimu duniani yanayofaa kwa uwekezaji wa viwanda vya kutengeneza malighafi hiyo ambayo inatumika kuzalisha kemikali mbalimbali.
SERIKALI inatarajia kutoa vibali vya kuajiri wafanyakazi 200 katika Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na zaidi ya asilimia 95 ya wafanyakazi hao wataongeza nguvu katika kutayarisha na kusimamia viwango vya ubora.
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema sekta ya utalii, itapiga hatua kubwa ya maendeleo, kama sekta binafsi itashirikishwa kikamilifu katika kuitangaza Zanzibar.
WAZIRI wa Fedha, Saada Mkuya Salum amesema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imejizatiti katika kuhakikisha inafanikiwa kwenye ukusanyaji wa kodi za ndani pamoja na kupata uzoefu wa sekta ya madini na gesi ili kuongeza manufaa zaidi.