DHAMANA ya Uwekezaji Tanzania (UTT) imeanza kutumia huduma ya MPesa katika kuwawezesha watanzania kununua vipande vya mifuko ya pamoja iliyopo chini ya UTT.
zaidi ya miaka 8 iliyopita
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kutekeleza uamuzi wake wa kuwapatia wakulima bei ya karafuu ya asilimia 80 ya bei ya zao hilo katika soko la nje.
KAMPUNI ya kimataifa ya Methanex ya Canada, inayotengeneza na kusafirisha malighafi ya methano imesema Tanzania ni moja ya maeneo muhimu duniani yanayofaa kwa uwekezaji wa viwanda vya kutengeneza malighafi hiyo ambayo inatumika kuzalisha kemikali mbalimbali.
SERIKALI inatarajia kutoa vibali vya kuajiri wafanyakazi 200 katika Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na zaidi ya asilimia 95 ya wafanyakazi hao wataongeza nguvu katika kutayarisha na kusimamia viwango vya ubora.
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema sekta ya utalii, itapiga hatua kubwa ya maendeleo, kama sekta binafsi itashirikishwa kikamilifu katika kuitangaza Zanzibar.
WAZIRI wa Fedha, Saada Mkuya Salum amesema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imejizatiti katika kuhakikisha inafanikiwa kwenye ukusanyaji wa kodi za ndani pamoja na kupata uzoefu wa sekta ya madini na gesi ili kuongeza manufaa zaidi.
BENKI ya Exim Tanzania imezindua mafunzo maalumu yanayolenga kuwapatia maofisa wake wapya na wa zamani wa matawi mbalimbali wa benki hiyo ujuzi katika shughuli za kibenki za miamala na juu ya sera za udhibiti ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja.
VIKUNDI 10 vya ujasiriamali vya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza vimekidhi vigezo vya kushiriki maonesho ya Wakulima ya Nanenane ya Kanda ya Ziwa yatakayofanyika eneo la Nyamhongo.
SERIKALI imeipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa kuboresha ukusanyaji wa mapato kupitia mfumo wa kielektroniki, ikiwa halmashauri ya kwanza nchini kufanya hivyo.
ZAIDI ya wateja 500,000 wameshajiunga na huduma ya M-pawa kufikia katikati ya Julai, mwaka huu, ikiwa ni miezi michache tangu huduma hiyo ilipozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwawezesha wananchi wengi zaidi kumiliki akaunti za benki.