OFISI ya Takwimu ya Taifa (NBS) imesema mfumko wa bei wa mwezi Julai, umeongezeka kidogo kutoka asilimia 6.4 ilivyokuwa Juni hadi asilimia 6.5.
zaidi ya miaka 8 iliyopita
WAKULIMA wameshauriwa kuchangamkia hati fungani za Serikali za muda mfupi na hata za muda mrefu ambazo, mbali na kuwasaidia kutunza pesa zao mahala salama, zitawapa faida pale zikapoiva na pia wanaweza kuzitumia kama dhamana ya mikopo ya pembejeo kwenye taasisi za fedha.
MWITIKIO wa wafanyabiashara kununua na kutumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFDs) umeongezeka kutokana na kupata elimu inayoendelea kutolewa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).
VYAMA vya msingi vya ushirika, mikopo na akiba mkoani Lindi, vimetakiwa visiwe vichaka vya viongozi wahalifu wa kuchota fedha na kuondoka.
KAMPUNI ya Swala Oil & Gas inayojihusisha na masuala ya uchimbaji wa mafuta na gesi, itajiorodhesha rasmi katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) keshokutwa.
KAMPUNI iliyoteuliwa kusambaza kinywaji cha Bavaria Afrika Mashariki, Jovet (Tanzania) Limited, imesema inaanza kujitanua kisoko nchini na Afrika Mashariki hivi karibuni.
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewaonya wadau wa kilimo cha pamba katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kwamba waache wivu, badala yake wamsaidie mkulima wa zao hilo ili aweze kuwa mshindani kwa nchi zinazolima pamba.
BENKI ya Twiga Bancorp, inatarajia kujitanua zaidi kwa kufungua tawi la sita kabla ya mwishoni mwa mwaka huu Kigamboni, Dar es Salaam.
SERIKALI ina mpango wa kuanzisha utaratibu wa kufuatilia magari yanayopeleka mizigo nje ya nchi kwa njia ya kielektroniki.
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda kesho Jumatano atafungua mkutano mkubwa unaohusisha wabunifu na wazalishaji kutoka nchi 10 za Afrika.